Wednesday, 14 March 2012

Historia ya BankKumekua na mshituko mkubwa kuhusu Bank za kiislam, sio tu kwa wasiokua waislam bali pia kwa baadhi ya waislam. Watu hawa wote wakiijuiliza maswali mbali mbali kama vile; Hivi kuna bank za kiislam?, zinafanya nini?, zinatumia mfumo gani wa kibiashara?, zilikua wapi siku zote?,hizi bank ni kwa waislam tu au kwa wasio waislam pia?, na maswali mengine mengi.

 
Ukweli ni kwamba fikra za kibank zilikuwapo ulimwengu mzima kwa sababu ni maumbile ya mwananadam kufikiria siku za baadae. kwa mfano mwanaadamu alikua na fikra za kuhifadhi vitu mbali mbali kabla ya kutumika kwa pesa. Itakumbukwa kwamba watu walikua wakihifadhi vyakula vyao, wanyama wao nakadhalika. Ilipo anzishwa fikra ya pesa kwa sababu tofauti binadamu alianza kuhifadhi pesa kwa mfumo mfinyu sana. kwa mfano wale waliojiamini walikua na sehemu maalumu ya kuhifadhia pesa zao, na wale wasiojiamini walikua na watu fulani wanao waamini kwahiyo waliwaomba kuhifadhi pesa zao.

Fikra hii ndio chimbuko la bank ambayo iliendelezwa kwa sura tofauti tofati kulingana na uwezo wa mwanaadamu, mahali alipo na mahitaji yaliyopo.  Fikra hii ilihama kutoka eneo kwenda eneo jengine kama tunavyoona sasa hivi kua tunatumia mfumo wa kibank wa kimagharibi. hebu tujiulize kwa mfano watawala wa kiAfrica kabla y wakoloni walikua wakihifadhi pesa zao vipi?. Hivi si kulikua na utawala wa kichifu ulioendesha serikali zao kulingana na mahitaji yao?. Ni kama hivyo basi waislamu walikua na mfumo wao wa kibank kabla ya kuingia ukoloni katika maeneo yao.
No comments:

Post a Comment