Tuesday, 13 March 2012

Maelezo ya bank za kiislam kwa ufupi


Benki za kiislam


Islamic Banking ni mipangilio mbali mbali na tofauti tofauti ya kibenki kama vile kuhifadhi pesa bank, kuchukua pesa kutoka bank, kusafirisha pesa kutoka bank kwenda bank nyengine, kusafirisha pesa kutoka nchi moja kwenda nchi nyengine , kufanya biashara kati ya mtu na mtu kwa msaada wa bank, kufanya biashara kati ya mtu kwa kushirikiana na bank, kukopa pesa kutoka bank na kadhalika na mipangilio hii yote inaendeshwa kwa mfumo wa kiislam.


kutokana na maelezo hayo ,tunaona kwamba bado kuna mambo mengi yanayohitaji kufafanuliwa. kwa mfano watu wengi watataka kujua nini hasa tofauti ya Bank za kiislam na zisizokua Bank za kiislam, ni mfumo upi huo unaotumiwa na Bank za Kiislam, nini tofauti ya mfumo huo wa unaotumiwa na bank za kiislam na ule unaotumiwa na bank zisizokua za kiislam? kwa upande mwengine tunaona kuna waislam wengi wanaweka pesa zao katika mabenk yasiotumia mfumo wa kiislam, na pia kuna wasiokua  waislam nao wanaweka pesa zao katika mabenk ya kiislam. kwa ufafanuzi zaidi fuatilia posts zinazofuata.

No comments:

Post a Comment