Friday 13 April 2012

Kitu gani kimepelekea kuzaliwa kwa benki za kiIslam

Bank za kiIslam ni kitu ambacho kilikuwepo na kitaendelea kuwepo ktk sheria ya kiIslam, ingawaje kutokana na mabadiliko makubwa ambayo yameikumba jamii kama vile kuongezeka idadi ya watu, mzunguko wa jamii kutoka kipindi fulani hadi kingine, kulikua na haja ya kurekebisha baadhi ya fikra ili kuweza kukabiliana na maendeleo makubwa ambayo binadamu anayashuhudia.

Uhakika ni kwamba vitu vingi vilishiriki ktk maendeleao ya bank za kiIslam, kwa mfano, muelekeo wa kimataifa wa kuzikumbatia banki zisizokua na riba na unaofanana na itikadi ya kiIslam ulioanza kujitokeza ktk kipindi takriban cha miaka thalathini iliyopita na matumizi ya ushirika (partnership) kama aina ya kibiashara ktk karne za kati ambayo baadae yalihamishiwa kwenye uIslam, yalikua na mchango mkubwa. Kwa upande mwingine kuna wale wanaodai kwamba utawala wa magharibi nao umeshiriki kwa kiasi fulani ktk kukua kwa bank za kiIslam.

Moja ktk fikra zilizopo ni pamoja na ile fikra ya kwamba presha iliyotokana na mfumo wa bank za kiMagharibi na ombwe lililokuwepo ktk uchumi wa kiIslam, viliwahamasisha wasomi wa kiIslam kujaribu kuulezea uchumi wa kiIslam kwa kutumia njia za kitaalam zaidi. Kwa mfano, sifa kubwa ya mfumo wa uchumi wa banki za kiMagharibi ulitegemea riba kwa kiasi kikubwa sana ambapo ilifikia kiwango hata cha kupuuza dini zao. Kitendo hicho kilizidi kukua kwa kiasi ambapo riba ilikua ni kama uti wa mgongo ktk uchumi wa Magharibi, kwa upande mwingine uIslam uliendelea kung’ang’ania kwamba riba sio sahihi.

Mapinduzi ya kiIslam ktk upande wa kiuchumi yaliamua kufuata mifumo ya kibiashara ambayo ilikubalika ktk dini yao kama vile kitu kinachojulikana kama (Mudarabah)na (Musharakah) ambazo zina maana ya kushirikiana kwa njia moja au nyingine, (Leasing) ambayo ina maana ya kukodisha na mifumo mingine mingi tu ya kiuchumi. Mifumo hiyo ya kiuchumi iliyotajwa itaelezewa kwa upana zaidi ktk makala zinazo kuja. Ktk kulifafanua hilo zaidi Shinsuke (2010) aliweka wazi kwamba, Uislam haukubali riba lakin unakubali faida, badala ya kutoa mikopo yenye riba, ni vyema bank zikafanya biashara na mteja na baadae wakashirikiana ktk hali mbili ima faida au hasara, na hilo halina kipingamizi ktk sheria ya kiIslam. Maneno hayo yamesomwa kutoka ktk kitabu cha Quresh kilichochapishwa mwaka 1945, ukurasa wa 158 hadi 159. Ktk makala zinazokuja tutafafanua zaidi mifumo ya biashara inayo kubalika kiIslam.

Kwa maelezo zaidi kwa yaliyozungumzwa unaweza kusoma

Shams, R. (2004), A critical Assessment of Economics, HWWA Discussion, Hamburg Institute of International Economics.

Shinsuke, N. (2010), Islamic Finance in Economic History: Marginal System or another Universal System? A paper presented at Second Workshop on Islamic Finance, France: EM Strasbourg Business School.



No comments:

Post a Comment