Monday, 9 April 2012

Uchumi wa soko huria (Free market)

Soko huria (Free market) ni aina nyingine ya uchumi ambao Karl Marx aliulezea kama uchumi ambao kikundi kidogo cha watu au wafanyabiashara ndio wanaomiliki kiasi kikubwa cha fedha, kuendesha kiasi kikubwa sana cha biashara na kufanya maamuzi mengi yanayohusiana na biashara. Maamuzi hayo ni kama bidhaa gani na huduma gani zizalishwe, wapi zipelekwe, nani apelekewe nani asipelekewe, bei ya bidhaa hizo na kadhalika. Serikali ktk nchi hizo ina nafasi ndogo sana katika biashara, kwa mfano, sio lazima kwa mfanya biashara kupata ruhusa maalumu kutoka serikalini.

Katika nchi za soko huria inadaiwa kua nadharia ya gawa kadri wanavyohitaji (Supply and demand) ndiyo inayoweka bei ya bidhaa, ugawaji, uzalishaji wa bidhaa, na mengineyo. Katika nchi hizo mara nyingi wateja wana sauti ya kuamua ni badhaa gani wanahitaji kuzinunua zizalishwe na kinyume chake, kwa maana hiyo biashara inategemea kwa kiasi kikubwa mahitaji ya wateja.

Ktk moja ya maswali yanayojitokeza ktk mfumo huo ni pamoja lile swali linalolouliza nini hasa jukumu la serikali katika mfumo wakibiashara kama huu? Jibu ni kama ifuatavyo; katika mfumo wakibiashara wa soko huria serikali inakua si mzalishaji mkubwa wa bidhaa na huduma, isipokua inabakia tu kua ni msimamizi wa uendeshaji wa biashara hizo ikiwemo utozaji ushuru, kuweka viwango vya bidhaa, na mambo mengine. Inasemekana kua Ujerumani,Uingereza, na Marekani ni mifano ya biashara huria duniani, ingawaje, hilo limekanushwa vikali sana na wataalamu wakibiashara duniani huku wakidai kua, nchi hizo hazifuati tena mfumo huo wa kiuchumi isipokua zinafuata mfumo mchanganyiki (mix economy).

Ni muhimu kukumbushana kwamba UIslam haupingani na aina yoyote ya uchumi ambao haitofautiani na maadili yake na unawasaidia waIslam kutatua matatizo yao. Isipokua uhakika unabakia kwamba uislam na uKomonist ktk maswala ya uchumi ni vitu viwili tofauti, ingawaje, kuna kufanana kukubwa ktk baadhi ya maeneo. Kwa mfano tukiangalia uKomonisti tunaona kwamba unapingana na uIslam ktk fikra (theory) na ktk utendaji (practical), na mgogoro wao ni wa lazima ambapo hauwezi kuepukwa. Kwa mfano uKomonist unaangalia sana upande wa material na sio kitu kingine chochote, na hii inatokana na kuamini kwao kwamba upande wa kiroho hauna maana yoyote. Kwa upande mwingine uIslam umekataa kumuangalia binadamu ktk mtazamo huo finyu kwakua unaamini kwamba, mahitaji ya binadamu hayaishii kwenye mahitaji ya kimwili peke yake kama vile chakula, makazi na maswala ya kijinsia kama alivyodai Karl Marx, isipokua mahitaji ya kiroho ni muhimu ktk swala zima la maisha ya binadamu ikiwemo uchumi.

Ni muhimu kutaja kwamba fikra ya uKomonist ya kuamini tu vitu vinavyoonekana (materialistic), ndio ambayo imewafanya waamini kwamba hakuna Mungu, mitume, wala vitabu na waliendelea kuamini kwamba vitu vyote vinatokana na mapambano ya nguvu za kiuchumi. Pamoja na mambo mengine sababu hiyo iliwafanya waKomonist wapuuze historia ya binandamu, na wakatae kutambua ujio wa uIslam kama mabadiliko ktk mfumo wa uchumi pamoja na kwamba uIslam ulileta mfumo tofauti wa kimaisha. Hii ni ushahidi wa kutosha kwamba uIslam unapingana na uKomonisti kinyume na madai ya baadhi ya waislam kwamba uIslam na uKomonist Hauna tofauti kabisa.
No comments:

Post a Comment