Friday 23 March 2012

Uchumi wa kiislam

Tunapozungumzia Uchumi wa kiislam, tunazungumzia vitu viwili ambavyo ni Uchumi na Uislamu. Uchumi ni harakati mbali mbali zenye malengo ya kuzalisha bidhaa na huduma mbali mbali, harakati hizi zinaweza kua katika eneo maalumu, pia zinaweza kuhama kutoka eneo kwenda eneo jengine. Ikumbukwe pia Uchumi ni neno pana sana na linaendelea kupanuka siku hadi siku, pia linatofautiana kutoka eneo kwenda eneo jengine, kwa mfano kitu fulani kinaweza kua ni uchumi eneo fulani, lakini kitu hicho hicho kisiwe uchumi katika eneo jengine.

Uislam ni dini yenye mfumo maalumu wa maisha ya kila siku ikiwemo mfumo wa kibiashara, kijamii, kiutawala nakadhalika, kwa maana hiyo tunapozungumzia uchumi wa kiislam, tunakusudia zile harakati mbali mbali zenye malengo ya kuzalisha bidhaa na huduma mbali mbali zilizopo katika mfumo wa kiislam. Hapa tunajifunza kua uislam una mfumo maalum wa kiuchumi ambao unakusanya vitu viwili muhimu ambavyo kulingana na sheria ya kiislam ni muhimu kuzingatiwa navyo ni Halali (acceptable) na Haram (forbidden).

Mfumo wa uchumi wa kiislam ni utaratibu ambao una malengo ya kutatua matatizo ya kiuchumi kwa kutumia maadili na sheria ambazo zimetokana na sheria ya kiislam. Kitu muhimu cha kukumbushana ni kwamba wakati mwengine sifa Kama hizi hukosekana ktk mifumo mingine ya uchumi, kwahiyo kuna umuhimu wa kutaja kua maadili mengi yaliyopo ktk uchumi wa kiislam yana uwezo wa kukubalika kwa walimwengu bila kulazimishwa.

Kwa mfano uislam unakataa fikra za (Mother Nature) ambayo inamaana kua dunia ilijiumba yenyewe, bali unaamini kua dunia na vyote vilivyomo ndani yake viliumbwa ispokua mwanadamu aliletwa kama muwakilishi wa Muumba na akapewa ruhusa ya kutumia vilivyomo duniani kwa uangalifu na kwa maslahi ya kizazi kinachokuja.

No comments:

Post a Comment