Tuesday 27 March 2012

Aina za kiuchumi

Mipangilio ya uchumi ni njia maalum ambayo nchi au Jamii fulani inazitumia katika kuulekeza vyanzo vyake vya kiuchumi ili kufikisha bidhaa na huduma mbali mbali kwa wananchi. Kulikua na njia za kiuchumi mbali mbali za kiasili ambazo zilikua ni kushirikiana jamii kwa kufanya kazi pamoja na kushirikiana faida au hasara na ilikua sio jambo zuri wakati huo mtu kufanya kazi peke yake kwa manufaa yake tu. Njia hizi za kushirikiana ziliendelezwa lakini siku hadi siku zilidumaa kwani mafanikio yake yalikua madogo na hapo ndipo baadhi ya watu wakaamua kulishughulisha swala la uchumi kwa kutumia juhudi binafsi. Inasemekan kua njia za kiuchumi za kizamani bado unaweza kuzikuta katika makabila yanayoishi nchini Australia, Amazon na baadhi ya nchi za Ulaya.

Njia za Uchumi zilipanuka siku hadi siku kitu ambacho ilikua ni sababu baadhi ya serikali kudhibiti njia hizo kwa kutumia njia mbalimbali kama vile kupanga matumizi, kushughulikia vyanzo vya uchumi na mengineyo ikiwemo kupanga mishahara ya wafanyakazi. Nchi zilizotumia mfumo huo zilijulikana kama nchi za kijamaa. Historia inaonyesha kua serikali nyingi za kijamaa zina utaratibu wa kudhibiti njia nyingi za kiuchumi kama vile viwanda vikubwa, kilimo cha kutumia nyenzo na nyenginezo. Mfano wa nchi hizo ni kama vile Soviet Union ambayo baada ya kusambaratika mwaka 1980 wameachana na mfumo huo. Aidha mfumo huo ulionekana kufuatwa na nchi nyingine kama vile Tanzania, Zimbabwe Syria ambazo wanaonekana kuuacha. Moja ktk nchi ambazo inaonekana kuendelea na mfumo huo ni Cuba.

Kuna nchi ambazo maamuzi ya kiuchumi sana yanafanywa na watu binafsi, kama vile bidhaa gani zizalishe, kiasi cha bidhaa hizo, soko, vyanzo gani vitumike, malipo yawe vipi na kadhalika. Nchi hizi zinajulikama kama nchi za soko huria ikiwemo Marekani ambayo iliamua kufuata mfumo huo tokea karne ya kumi na tisa. Baadae kuna nchi ambazo zinachanganya kati ya aina hizo mbili za kiuchumi. Kwa mfano kuna baadhi ya maeneo ya kiuchumi yanayodhibitiwa na serikali, na maeneo mengine yanaendesha na watu binafsi huku serikali ikichangia kwa kiasi kikubwa na kutoa maelekezo ni jinsi gani vyanzo vya kiuchumi Vitumike. Ni muhimu kukumbushana kua Marekani ya leo ni moja kati ya nchi ambazo zinafuata mfumo huu wa kiuchumi. Moja ktk maswali yanayojitokeza ni pamoja na vipi vitega uchumi vya serikali na vya watu binafsi vinaweza kufanya kazi pamoja bila kuathiri uchumi wa nchi husika? Inasemekana kua moja katika athari yake ni hii inayoonekana leo ya kuporomoka kwa uchumi Duniani. Makala zinazokuja zitafafanua zaidi

No comments:

Post a Comment