Thursday, 15 March 2012

Historia ya bank za kiislam no 3

Tunapozungumzia bank za kiIslam tunazungumzia matumizi ya bank baada ya ujio wa mtume Muhammad (SAW). Ni kweli kabisa kua wakati wa mtume Muhammad waIslam walikua na mfumo wao maalum wa kibank. Mfumo huu uliendelea mpaka iliposamabaratika dola la mwisho la waIslam ambalo ni Othman empire.
Ikumbukwe kwamba matumizi ya kibank pia yalikuwepo katika tawala nyengine kama vile Roman Empire na Pesia katika mifumo tofauti tofauti na ile ya kiIslam. Lakini mifumo yote hiyo ile ya kiIslam na isiyo ya kiIslam ilikuwa na malengo yanayofanana . Kama tulivyoeleza huko nyuma kua mifumo ya kibank ilihama kutoka eneo kwenda eneo nyengine kama ilivyo kawaida ya tamaduni nyingine, kwahiyo Utamaduni wa kibank za kiIslam unaundwa na tamaduni mbali mbali zikiwemo za Roman na Pesia.
Kutokana na hayo tuliyoyaeleza utakuta kua historia ya benk za kiIslam kama zilvyo sasa inaweza kugawika ktk sehemu mbili muhimu. Sehemu ya kwanza ni ile ya (Theory) fikra na sehemu ya pili ni ya vitendo (practical). Kwa muda mrefu tangu kuanguka kwa Othman empire bank za kiIslam zilikua ni Fikra (Theory) tu kuliko Matumizi (Ptacticle) . kwa maana hiyo utakuta kwamba waislam wengi walitumia mabenk yanayofanya kazi katika mfumo wa kiMagharibi.Bank za kiislam kwa mfumo huu uliopo zilianza kwenye miaka ya 1946, 1948 na 1952. Hii ilikua ni baada ya baadhi ya wasomi wa kiIslam kuyazungumzia kwa kina zaidi maoni ya uislam ktk swala zima la biashara, mmoja kati ya wasomi waliotua juhudi kubwa alikua ni Abu Al alaa  Al Maududi mwaka 1950.
Wasomi wengi waliona ipo haja ya kuanzisha (commercial bank) na walichagua ushirika kati ya bank na mteja (Mudarabah) itumike kama njia ya kuziendesha bank hizo ambapo mteja atashirikiana hasara au faida na bank. Mudharabah ni  maana yake ni kusafiri, lakin ktk lugha ya biashara ni biashara ambayo wanashirikiana watu wawili au zaidi. Upande mmoja unatoa mtaji wa biashara na mwengine anahangaika kufanya biashara baadae, wanagawana faida kwa asilimia watakazokubaliana kabla ya kuanza biashara na kama ikipatikana hasara muhangaikaji anapoteza nguvu zake na alietoa mtaji kama ni bank au mwengine yoyote anapoteza mtaji wake. Maana ya mudarabah itazungumziwa kwa ufasaha zaidi kama mada tofauti ktk makala zinazokuja.
Kwenye mwaka 1970 mawaziri wa uchumi wa nchi za kiislam walifanya mkutano Karachi mji mkuu wa Pakistan, ulifuatiwa na mkutano wa 1972 uliofanyika Egypt nchini Misri na mikutano mingine ilifanyika Mecca Saudi Arabia na London uingereza na hapo ndipo bank ya kwanza ya kiislam kwa jina la (Islamic Development bank) na inter-government bank zilipoanzishwa mwaka 1975.Vilevile zilianzaishwa bank za watu binafsi za kiislam nchini Dubai mwaka 1975 na kundi la wafanya biashara kutoka nchi mbalimbali, na nyingine zikaanzishwa Egypt na sudan. Ktk miaka ya sitini Serikali ya Malysia Ilianzisha mfuko maalum kwa ajili ya Hijja (kwenda Makkah kutekeleza ibada ya kuhiji) ambapo mfuko huo ulikua na malengo ya kuhifadhi pesa na kuzizalisha kwa kutumia biashara mbalimbali za zinazokubalika kiislam. Bank nyingine ilanzishwa ktk mji wa Mit-ghamr  nchini Misri lakin baadae ilifungwa kwa sababu mbalimbali na badala yake Nasir social bank ilianzishwa mwaka 1972.
Baada ya miaka kumi kuanzishwa bank hizo, hivi sasa kuna bank karibu zaidi ya hamsini na nyingi ziko ktk nchi zenye waislam wengi, bank  nyingine ziko ktk nchi za ulaya magharibi kama vile Denmark, Luxembourg, Switzerland na United Kingdom. Itakumbukwa kwamba kuna mikutano mingi ambayo imefanyika kujadili bank za kiislam kama ule uliofanyika Washington D.C mwezi wa tisa mwaka 1986, Geneve mwezi wa kumi1986, London mwaka 1988 na Islamabad nchini Pakistan mwaka 1992.
Ni muhimu kueleza kwamba kwa sasa banki za kiislam zimetanua wigo wa huduma zake na zinakua kwa kasi zaidi. maelezo zaid yatafuatia ktk mada zinazokuja.
Kuna dhana nyingi ambazo zina utata kua bank za kiislam zinazungumzia riba na kushirikiana ktk hasara na faida tu. Ukweli ni kwamba kuna huduma nyingi zinazotolewa na bank za kiislam na kuna huduma nyingi ambazo bank za kiislam na zisizo za kiislam zinashirikiana. Mada zinazokuja zitaweka wazi zaidi.

Kwa maelezo zaidi soma Abdul Ghafoor, A. (1995) ISLAMIC BANKING This is actually Chapter 4 of the book, Interest-free Commercial Banking, by the author, 1995.


2 comments:

  1. Hi I am Emm just testing the blog. thks

    ReplyDelete
  2. now it's ok to comment.

    ReplyDelete