Thursday, 5 April 2012

Uchumi wa kijamaa: Communism

Ujamaa:(Communism) ni imani ya kisiasa na kiuchumi ambayo wafuasi wake wanataka watu wote wanoishi katika jamii fulani (wamiliki kwa pamoja) na kusiwe na matabaka kati ya watu wa jamii hiyo. Watu wa Uchumi na siasa wengi wanaamini kua, wajamaa wengi ni kama alivyo muanzilishi wao Karl Marx wanaamini kwamba maisha ni kiasi cha mvutano kati ya wafanyakazi, wenye viwanda na makampuni. Vilevile wanaamini kua Ujamaa kinyume chake ni Ubepari ambao imani yake ni kwamba, watu wanatakiwa wapate kadri wanavyofanya na kushirikiana ktk jamii hakuna umuhimu wowote, ispokua watu wa jamii fulani wanaweza kushirikiana pale wanapokubaliana kufanya hivyo. Ktk upande wa uchumi serikali za nchi za kijamaa ndizo zinazomiliki njia zote za kiuchumi, na watu wengine au mashirika binafsi wanatakiwa wapate ruhusa maalum kutoka serikalini ili waweze kufanya biashara.

Imedaiwa kwamba katika nchi za kijamaa bidhaa zinatengenezwa kadri ya mahitaji tu, na serikali ndio inayohusika ktk kuweka utaratibu wote kuhusu bidhaa hizo. Kwa mfano serikali ndio inayoamua wapi bidhaa hizo zipelekwe, nani apelekewe na nani asipelekewe, nakadhalika. Mfano mzuri wa kiuchumi wa kijamaa ktk wakati tulionao ni ule wa kule nchini Quba. Ikumbukwe ya kwamba nchi kama Quba na nchi za kijamaa nyengine, serikali ndizo zinayomiliki viwanda,mashirika,ardhi, ushuru wa forodha na njia zote kuu za kiuchumi. Inadaiwa kua Ujamaa wa kweli katika uchumi hauruhusu watu binafsi kumiliki mali, na kwa sababu hizo nchi za kijamaa zinahitaji serikani kubwa, pana, yenge nguvu na makini sana, kwa sababu serikali inatakiwa kudhibiti kila kitu kama vile aina ya bidhaa, bei ya bidhaa, viwango na kadhalika.

Tukumbushe kua watu wengi wasio wachumi wanafikiri kua nchi kama China bado inafuata mfumo wa kiuchumi wa kijamaa, ukweli ni kwamba serikali ya China imeziachia baadhi ya biashara kwa watu na mashirika binafsi. Kama tulivyoona uchumi wa kijamaa kua umeachwa na nchi nyingi hapa duniani, Wanauchumi wengi wanadai kua bado kuna mazuri mengi katika mfumo huu wa kiuchumi, ingawaje hayo yapepingwa vikali sana na wana uchumi wengine.


No comments:

Post a Comment