Showing posts with label Islamic Economics. Show all posts
Showing posts with label Islamic Economics. Show all posts

Friday, 23 March 2012

Uchumi wa kiislam

Tunapozungumzia Uchumi wa kiislam, tunazungumzia vitu viwili ambavyo ni Uchumi na Uislamu. Uchumi ni harakati mbali mbali zenye malengo ya kuzalisha bidhaa na huduma mbali mbali, harakati hizi zinaweza kua katika eneo maalumu, pia zinaweza kuhama kutoka eneo kwenda eneo jengine. Ikumbukwe pia Uchumi ni neno pana sana na linaendelea kupanuka siku hadi siku, pia linatofautiana kutoka eneo kwenda eneo jengine, kwa mfano kitu fulani kinaweza kua ni uchumi eneo fulani, lakini kitu hicho hicho kisiwe uchumi katika eneo jengine.

Uislam ni dini yenye mfumo maalumu wa maisha ya kila siku ikiwemo mfumo wa kibiashara, kijamii, kiutawala nakadhalika, kwa maana hiyo tunapozungumzia uchumi wa kiislam, tunakusudia zile harakati mbali mbali zenye malengo ya kuzalisha bidhaa na huduma mbali mbali zilizopo katika mfumo wa kiislam. Hapa tunajifunza kua uislam una mfumo maalum wa kiuchumi ambao unakusanya vitu viwili muhimu ambavyo kulingana na sheria ya kiislam ni muhimu kuzingatiwa navyo ni Halali (acceptable) na Haram (forbidden).

Mfumo wa uchumi wa kiislam ni utaratibu ambao una malengo ya kutatua matatizo ya kiuchumi kwa kutumia maadili na sheria ambazo zimetokana na sheria ya kiislam. Kitu muhimu cha kukumbushana ni kwamba wakati mwengine sifa Kama hizi hukosekana ktk mifumo mingine ya uchumi, kwahiyo kuna umuhimu wa kutaja kua maadili mengi yaliyopo ktk uchumi wa kiislam yana uwezo wa kukubalika kwa walimwengu bila kulazimishwa.

Kwa mfano uislam unakataa fikra za (Mother Nature) ambayo inamaana kua dunia ilijiumba yenyewe, bali unaamini kua dunia na vyote vilivyomo ndani yake viliumbwa ispokua mwanadamu aliletwa kama muwakilishi wa Muumba na akapewa ruhusa ya kutumia vilivyomo duniani kwa uangalifu na kwa maslahi ya kizazi kinachokuja.

Tuesday, 20 March 2012

Uchumi

Mwanadamu amepata tabu sana na mambo ya kiuchumi tangu kuumbwa kwake. Inaonekana uchumi hakikua ni kitu kinachojulikana maelezo yake kwa uhakika, ingawaje, uchumi ulifahamika kama swala la kumuwezesha mwanadamu kuishi na kupata mahitaji yake fulani fulani na kuweza kujiendeleza.
Kuna maoni tofauti tofauti nini hasa maana ya kujiendeleza, kuna wale wanaoona kwamba kujiendeleza maana yake ni kupiga hatua ktk mambo yanayoonekana (Materialistic), kama ni hivyo basi, malengo ya binadamu au jamii yataelekeza juhudi zake kwenye kupata mahitaji yake binafsi na ikiwezekana kujilimbikizia  utajiri mkubwa. Hali ikiwa hivyo ni dhahiri kwamba, malengo yote na huduma zote  zinakua ni  kwa ajili ya mtu kupata maslahi binafsi na watu watakua hawana malengo ya pamoja, na kama yapo basi yatapuuzwa na kila mmoja atakua na uhuru wa kuamua kitu gani ana maslahi nacho zaidi.
Lakin kama kutakua na malengo ya kibinadamu au ya kiitikadi basi malengo ya uchumi ya jamii hiyo, yatashughulikia sana usawa ktk jamii, ajira na kugawana utajiri kwa malengo ya kunyanyajua kipato cha jamii kwa ujumla. Ni muhimu kutaja kua malengo ya kiuchumi ya jamii Fulani yatategemeana na mahitaji ya jamii hiyo.
Makala zinazokuja zitaelezea kwa ufasaha zaidi maswala aina za uchumi.