Events/Matukio

IMF, World Bank acknowledge Islamic finance as powerful development tool for members February 28 2017 09:28 PM
By Arno Maierbrugger/Gulf Times Correspondent /Bangkok

Islamic finance continues to take the centre stage at global financial institutions. In early February, the International Monetary Fund’s (IMF) executive board held its first formal discussion on Islamic finance and adopted a set of proposals on the role that the IMF should play in this area. The fund concluded that Islamic finance presents an opportunity for many member countries to enhance financial intermediation and inclusion and mobilise funding for economic development. To utilise this potential, the fund says that there was a necessity to establish “a policy framework that promotes financial stability and sound development of Islamic finance in order to reduce systemic risks.”
In particular, the IMF saw merit in considering a proposal to formally recognise the “Core Principles for Islamic Finance Regulation for Banking,” prepared by the Islamic Financial Services Board, as a standard for the industry.
“We are looking forward to receiving a formal proposal for endorsement in the context of a forthcoming paper before end-April 2018,” the IMF says in a statement.

“We support the approach to developing and providing policy advice on Islamic banking-related issues in the context of fund surveillance, programme design and capacity development activities. We also support the work of the relevant international standard setters and other international bodies to help address current gaps in the international regulatory framework for Islamic banking,” the statement said.
Shortly after the IMF released its assessment of Islamic finance, the World Bank and the Islamic Development Bank (IDB) published their first “Global Report on Islamic Finance,” subtitled “A Catalyst for Shared Prosperity?” which focuses on the prospects of the global Islamic finance industry and its potential to help reduce worldwide income inequality, enhance and share prosperity, as well as achieve the United Nation’s Sustainable Development Goals.

“The report has been prepared with a focus on the widening disparity of global wealth and how Islamic finance can help in enhancing shared prosperity,” says Ahmed Mohamed Ali, president of the Islamic Development Bank Group.
“Given its potential role in economic development, Islamic finance can contribute toward achieving objectives of minimising disparity in wealth and enhance shared prosperity in order to reduce severe inequality that adversely affects economic growth and wealth creation and imposes social and environmental costs,” he adds.

The report is based on the assumption that Islamic finance advocates for just fair and equitable distribution of income and wealth. Unlike conventional finance, Islamic finance is based on risk-sharing and asset-based financing. By making people direct holders of real assets in the real sector of the economy, it reduces their aversion to risk. And the strong link to the real economy is another core benefit. With those principles, Islamic finance could help improve the stability of the financial sector, the reports notes.
Apart from that, Islamic finance plays an important role in enhancing financial inclusion as it can bring into the formal financial system people who are currently excluded from it owing to cultural or religious reasons.
But, just as the IMF, the World Bank/IBD report points at the importance of establishing a strong regulatory regime to reach the full potential of Islamic finance. There should also be mechanisms in place to enhance harmonisation, implementation and also provide regulatory recognition of products from other jurisdictions to expand the markets through cross-border transactions, the report recommends.
It also advocates the creation of institutions that provide credit and other information to support equity-based finance, particularly for micro, small and medium-sized enterprises, and further develop capital market products and sukuk to help finance large infrastructure projects.
To achieve all these goals, Islamic finance should “go beyond banking,” the report notes, and support non-banking institutions which are currently underdeveloped or underutilised. This includes takaful operators with their risk-sharing, participation-based Islamic insurance products, as well as social finance organisations which could alleviate poverty by tapping into the potential of zakat and waqf, Islamic principles rooted in redistribution and philanthropy.





Nchi ya Kenya imeziangalia upya sheria zinazo husu benki zinazo fuata maadili ya ki Islam ili iweze kuzijengea mazingira kufanya kazi zake vizuri. Pamoja na mambo mengine waliangalia uwezekano wa kuruhusu hati fungani {bond) inayofuata maadili ya ki Islam (Sukuk) kama alivyo sema mwanasheria wake mkuu.

Nchi hiyo ambayo ilianza Eurobond mwaka 2014 inataka kutanuwa wigo wake ili kuendeleza miundo mbinu kama vile barabara na biashara nyingine kubwa kubwa. Waziri wa fedha wa nchi hiyo amesema anaangalia uwezekano wa kuanzisha hati fungani inayo fuata maadili ya ki Islam ktk mwaka wa uchumi 2016/2017. Mkuu huyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba anategemea shughuli hiyo inaweza kukamilika ktk kipindi cha takriba miezi tisa.



MATUNDA YA BIMA INAYOFUATA SHERIA ZA KI-ISLAM

Moja ktk  tofauti kubwa iliyopo kati ya bima inayofuta sheria za ki-Islam na ile isiyofuata sheria ya ki-Islam ni kitendo cha wateja kugawiwa faida inayopatikana ktk biashara hiyo.
Takaful Insurance of Africa Limited (TIA) ni shirika la bima la kwanza nchini Kenya linalofuata sheria za ki-Islam ambalo limetangaza kugawana faida na wateja wake. Ktk kongamano lililohudhuriwa na mashirika yasiyopungua 500 ambayo ni wateja, brokers na mawakala, TIA ilitangaza kugawana asilimia 60 ya faida na wateja wake 4000 ambao hawakudai fidia yoyote ktk kipindi cha mwaka mzima. Alinukuliwa akisema mwenyekiti wa shirika hilo ndugu Abdurahman Sheikh ‘ninayo furaha na heshima kubwa kutangaza kwamba TIA imepata ziada (Surplus) yake ya kwanza ambayo ni sawa na Sh 15.6 million za Kenya na ambazo watagawana na wateja wake’, ktk tukio ambalo ni lakwanza kwa shirika la bima kufanya hivyo Kenya na Africa Mashariki kwa ujumla.
Akizungumza ktk kongamano hilo Mkurugenzi Mkuu Ndugu Hassan Bashir alisema ‘shirika limekua sana ukilinganisha na lilivyoanzishwa miaka miwili iliyopita, na limeweza kufanya kwa kipindi hicho, kile ambacho mashirika mangine yamekifanya kwa muda usiopungua miaka kumi’. Kwa maelezo zaidi kuhusu bima inayofuta sheria za ki-Islam wasiliana na http://ijuebankyakiislam.blogspot.com  



DUBAI INA MATEGEMEO MAKUBWA YA KUA KITIVO (HUB) YA UCHUMI UNAOFUATA SHERIA ZA KI-ISLAM

Wakati ulimwengu ukiyumba kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi, wajasiri mali wanatafuta uchumi mbadala ambao wanaweza kuuamini kwa ajili ya kuhifadhi na kuzalisha pesa zao.

Ktk mazingira hayo kuna sababu nyingi za kuamini kwamba uchumi unaofuata sheria za ki-Islam unajiuza, na hilo limetokana na misingi yake ktk kukataa riba, kukataa kitu kinachijulikana kama ‘short selling na baadhi ya miamala ya kibiashara inayoendelea duniani. Ni kwa sababu kama hizo ambapo ulimwengu uliingia ktk matatizo makubwa ya kiuchumi na kwa ajili ya kutaka faida nyingi na kwa kipindi kifupi, kwa ajili hiyo wajasiri mali wanatafuta uchumi ambao unaongozwa kwa misingi madhubuti na kwa umakini wa hali ya juu imefahamika.

Kufuatia mazingira hayo kiongozi wa Dubai Sheikh Mohammad Bin Rashid Al Maktoum mapema mwaka huu ametangaza kwamba ana mpango wa kuifanya Dubai kuwa makao makuu ya uchumi unaofuata sheria za ki-Islam.

Kama hatua ya kulifanikisha hilo Sheikh Rashid alitangaza plan ya kuibadilisha Dubai kua makao makuu ya Sukuk (Islamic bonds) ambazo zitahamasisha mashirika na nchi mbalimbali kutoa Islamic bonds badala ya zile zile zisizokua za ki-Islam. Ktk hatua nyingine ni kuundwa kwa jopo la kisheria la pamoja ambalo litashughulia na maswala ya viwango. Kwa maelezo zaidi kuhusu benki zinazofuata sheria za ki-Islam tembelea http://ijuebankyakiislam.blogspot.com





KENYA INAPIGA HATUA NYINGINE KWENYE UCHUMI UNAOFUATA SHERIA ZA KIISLAM

Kenya imepiga hatua nyingine ktk uchumi unaofuata sheria za ki-Islam kwa kuanzisha Reinsurance window inayofuata sheria za ki- Islam inayojulikana kama (Retakaful). Akifungua huduma hiyo wiki iliyopita Mkurugenzi mkuu Jadia Mwarania alisema ‘shirika limeamua kuchukua hatua hiyo ili ukabi;iana na mahitaji ya huduma zinazofuata sheria ya ki-Islam’. Aliendelea kusema ‘tunaiona hii kama fursa kubwa ya biashara ambayo thamani yake ni sawa na Dola billion kumi za Marekani kwa ulimwengu mzima na inaendelea kukuwa’.

Kwa upande mwengine mkurugenzi huyo alisisitiza kwamba biashara hiyo atahahakisha inakamilisha masharti yanayotakiwa ili iwe halali kwa sheria za ki-Islam. Aliwataja wasomi walio bobea na ambao wanategemewa kuisimamia biashara hiyo kwamba ni Pro Muhammad Salim Badamana wa chuo kikuu cha Nairobi, Muhammad Ali ambae ni muhadhiri ktk chuo cha Thika College for Sharia and Islamic Studies na Mwanakombo Noordin ambae ni mkurugenzi wa chuo kikuu cha Moi Coast Campus. Kwa maelezo zaidi kuhusu benki zinazofuta sheria za kiislam usikose kutembelea www.ijuebankiyakiislam.blospot.com



BANK INAYOFUATA SHERIA ZA KIISLAM ‘AL BARAKA’ IMEANZISHA HUDUMA ZA ‘FOREIGN EXCHANGE’ NCHINI AFRICA YA KUSINI

Bank inayofuata sheria za ki-Islam nchini Africa ya kusini inayo julikana kama Al Baraka imeanzisha huduma za ‘foreign exchange’.
Mkurugenzi mkuu wa benki hiyo ndugu Shabir Chohan alinukuliwa akisema ‘chini ya huduma hiyo ambayo ni mpya kwa benki hiyo, itaiwezesha kutoa huduma za kibenki sawa na zile za kimataifa ambapo wateja wao watafaidika na yale ambayo walikua wakiyakosa kwa muda mrefu’. Alifafanua kwamba benki zinazofuta sheria za ki- Islam, ziliruhusiwa kutoa huduma fulani fulani kama vile kuuza na kununua fedha za kigeni bila kutoza gharama zozote tangu mwaka 2008.
Huduma hiyo na hudum nyingine kama ile ya kutoa chequebook, itaiweka benki hiyo ktk nafasi nzuri ya ushindani wa kibiashara nchini humo.
Kwa maelezo zaidi kuhusu benki zinazo fuata sheria za ki-Islam tembelea www.ijuebankyakiislam.blogspot.com



BENKI ZINAZOFUATA SHERIA ZA KIISLAM ZINAZIDI KUENEA

Kitengo kinacho shughulika na ukuaji wa benki za ki-Islam The Islamic Corporation for the Development of the Private Sector (ICD) kina mpango wa kufungua benki mpya ktk nchi za Mali na Benin mwaka huu 2013.Mkurugenzi mkuu wa ICD Mh. Khaled Mohammed Al- Abood akizungumza ktk mkutano unao husiana na benki hizo uliofanyika nchini Djibouti, alinukuliwa akisema kwamba ICD itausaudia uchumi huo ktk maeneo ambayo bado huduma zake ni ndogo. Ktk kulifafanua hilo alisisitiza kwamba shirika hilo lina mpango wa kutoa million 200 Sukuk (Islamic bonds) kwa serikali ya Senegal kwa ajili ya kuiwezesha nchi hiyo kutoa huduma ya benki zinazofuta sheria ya kiislam.

Alinukuliwa akisema ‘zaidi ya asilimia 50 ya wakazi wa Africa ni waislam na mahitajio ya huduma hiyo ni makubwa sana lakin kuna changamoto nyingi zinazohusiana na kufika kwa huduma hiyo ktk maeneo husika. Tabia ya benki zinazofuata sheria za ki-Islam zinaiweka ktk nafasi nzuri ya kua mbadala wa benki zisizofuata sheria za ki- Islam na ambazo zimekuwepo kwa muda mrefu.

ICD ilikua na matumaini makubwa ya kufanya miradi mingi Africa kwa kua inafahamu kwamba Africa inahitaji sana miundombinu. ‘Kitu ambacho nchi za Afrika inakihitajia sana kwa ajili ya maendeleo ni miundombinu, barabara, nyumba, mashule na hospitali’ alisema ndugu Al-Abood.Karibu nchi kumi barani Africa zimeshakubaliwa kupata msaada wa ICD kati ya mwaka 2010-2012 na kuna zile ambazo zimefaidika sana kama vile Mauritania, Sudan, Gabon, Gambia na Mali.


UCHUMI UNAOFUATA SHERIA ZA KIISLAM UTAISADIA SANA AFRICA KUENDELEA KIUCHUMI

Kwa zaidi ya miaka kumi biashara kati ya Africa na ulimwengu kwa ujumla imekua sana, wakati ambapo biashara kati ya Africa na nchi za Gulf Cooperation Council (GCC) imekua kwa asilimia 170. Mabadiliko yaliyo zikumba nchi za Africa kutoka kwenye nchi tegemezi na kuelekea kwenye nchi za kibiashara, na uhusiano uliopo kati ya nchi za Africa na Mashariki ya Kati, imeuweka uchumi unaofuata sheria za kiIslam ktk nafasi muhimu ya kuandaa mazingira ya biashara kati ya Africa na nchi hizo. Umuhimu huo unaongezeka zaidi kwa sababu ya uhusiano mkubwa uliopo kati ya uchumi unaofuta sheria za kiIslam, biashara (real economic activity) na vyanzo vilivyopo ambavyo vinatoa mwanya wa biashara ktk nyanja muhimu kama vile Small and Medium Enterprises (SMEs). Hamu kubwa ya wajasirimali wa Mashariki ya kati ktk biashara kama za kilimo, kununua ardhi na viwanda, kunategemewa kukuza kwa kiasi kikubwa uchumi wa bara la Africa.



TUNISIA INA MPANGO WA KUANZISHA DHAMANA (BONDS) INAYOFUATA SHERIA YA KIISLAM

Nchi ya Tunisia ina mpango wa kutoa dhamana (bonds) zinazofuta sheria za kiIslam mapema mwaka 2013. Nchi hiyo ina mpango wa kurekibisha mfumo wake wa kibenki ili uwe na vyanzo mbalimbali vya uzalishaji kwa mujibu wa governor wa benki kuu ndugu Chadi Ayari.
Tunisia itatoa dhamana hizo mapema mwaka ujao kama sehemu ya budget yake ya mwaka 2013. Kuna utafiti unaendelea kuhusu uchumi zinazofuata sheria za kiIslam ikiwemo swala la kutoa dhamana. Committees ilioandaliwa na waziri wa fedha, waziri wa mambo ya dini na benki kuu ya Tunisia zinafanya kazi usiku na mchana ili na kuanazisha benki zinazofuata sheria za kiIslam, nchi ambayo hadi sasa ina benki mbili tu za kiIslam.
Mkurugenzi mkuu wa benki kuu ya Tunisia Nadia Kamba aliwaambia Reuters ‘sheria itakua tayari ktk kipindi cha wiki fulani na baadae itapelekwa serikalini kwa ajili ya kuidhinishwa’.


AUSTRALIA INAHARAKISHA KUUKARIBISHA UCHUMI UNAOFUATA SHERIA ZA KIISLAM

Serikali ya Australia itapeleka kundi la wataalamu nchini Dubai kwa ajili ya kujadili njia za kuendeleza uchumi unaofuata sheria za kiIslam nchini Australia. Ujumbe huo utakaongozwa na mtaalamu wa kiuchumi wa Australia ndugu Barry O’Farrell na wataalamu wengine wa mambo ya kiuchumi, watajadili maswala mazima yanayohusiana na usimamizi na sheria za uchumi huo, wakati huohuo ujumbe huo utatembelea mji wa Abu Dhabi na Lebanon.

Australia ina mategemeo ya kua na mchango mkubwa ktk uchumi huo kwa kuzingatia kwamba nchi za kusini mashariki mwa Asia ambazo zina uhusiano wa karibu na nchi hiyo, uchumi unaofuata sheria za kiIslam unakua kwa kasi. Moja ktk matatizo yaliyopo ni pamoja na uhakika kwamba juhudi za kupitisha sheria ya kuuruhusu uchumi huo kasi yake ni ndogo sana ktk ngazi za juu, kitu ambacho kimeilazimisha serikali ya Australia kuingilia kati. Serikali ya Austaralia ina hamu kubwa ya kujihusisha na uchumi huo alisema Salim Farrar muhadhiri mkuu wa kitengo cha sheria ktk chuo kikuu cha Sydney ambae alikiri vilevile kwamba swala hilo linahitaji mtiririko wa majadiliano ya kisiasa.

Pamoja na mambo mengine Australia inakabiliana na changamoto zinazohusiana na sheria mpya za uchumi unaofuata sheria za kiislam hususan ktk maswala mazima ya Islamic bonds na triple tax duties. Kwa maelezo zaidi wasiliana na http://ijuebankyakiislam.blogspot.com



BENKI INAYOFUATA SHERIA ZA KIISLAM INAPIGA HODI NCHINI UJERUMANI

Shirika la Turkey’s Kuveyt Turk investment lina mpango wa kufangua benki ya kwanza inayofuata sheria za kiislam nchini Ujerumani. Shirika hilo lina mpango wa kufanya hivyo mwezi wa kumi mwaka huu 2012 kwa matumaini kwamba athari mbaya zinazotokana na uchumi wa nchi za ulaya, zinaweza kupunguzwa na benki hizo ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa.

Muasisi na mkurugenzi wa Institute for Islamic Banking and Finance (IFIBAF) ndugu Zaid el- Mogaaddedi aliopo ktk mji wa Frankfurt nchini Ujerumani, alinukuliwa akisema ‘fikra nzima ya benki zinazofuata sheria za kiIslam ni kufuata maelekezo na kanuni za kiIslam.

Benki zinazofuata sheria za kiIslam zimeanzishwa nchi mbalimbali ktk bara la ulaya lakini wataalamu wa kiuchumi wamekadiria kwamba benki hiyo inaweza kufanikiwa sana nchini Ujerumani kuliko ilivyofanikiwa nchini Ufaransa na uingereza. Changamoto kubwa ni ile inayohusiana na uwezo wa benki za kiIslam kua na miundombinu na huduma nzuri alisema El-Mogaddedi.

Ujerumani ina idadi ya Waislam milioni 3, 8 hadi 4,3 ambao ni sawa na asilimia tano ukilinganisha na idadi ya wakazi wa Ujerumani ambao idadi yao ni milioni 82. Benki hiyo inawalenga waislam na wasiokua waislam. Uchumi unaofuata sheria za kiIslamu ni ktk moja ya uchumi ambao unakua kwa haraka sana duniani. Ktk jumla ya sababu za kukua kwa uchumi huo, ni pamoja na Waarabu kuondoa pesa zao nchini marekani na kuziweka ktk nchi za kiIslam ikiwemo Malysia na bara Arabu, baada ya uvamizi maarufu unaojulikana kama 9/11, ikifuatiwa na uchumi huo kuingiza faida ktk kipindi ambacho uchumi wa dunia ulitetereka.





BIMA INAYOFUATA SHERIA ZA KIISLAM (TAKAFUL) KUSHINDA NCHINI KENYA

Bima inayofuata sheria za kiIslam inayojulikana kama (Takaful) imekua mshindi ktk mkutano wa tatu unaofanyika kila mwaka nchini Kenya na ambao umefanyika kwa mara ya tatu mwaka huu. Wakati wanatoa zawadi hiyo waamuzi wa kikao hicho ilibainika kwamba ilikua ni mara ya kwanza ambapo zawadi hiyo imekwenda kwa shirika jipya, shirika ambalo limeanza kazi zake mwezi wa tatu mwaka huu 2012. Ni muhimu kukumbushana kwamba hilo ni shirika la kwanza ambalo linafanya kazi zake kwa kufuata sheria za kiislam. Walisikika wakisema wamiliki wa shirika hilo ‘Tumefurahi na tunahisi faraja kupata zawadi hii. Tukio hili linazungumza kwa sauti ya juu kwamba kazi zetu zimehishimiwa na mashirika mengine ya bima alisema CEO Hassan Bashir’. Kupata zawadi kama hii ni ushahidi wa wazi kwamba masharti muhimu kama vile uwazi, heshima, kukubali majukumu ni muhimu ktk biashara ya bima. Mkutano huo wa mwaka unaandaliwa na business intelligence na publishing house Think Business Limited.
Fikra ya bima inayofuata sheria za kiIslam ni kushirikiana na kusaidiana na kudhaminiana. Pamoja na mambo mengine bima ya kiIslam inakataza aina zote za mambo ambayo yatakua na uhusiano na riba, kamari na hadaa.
Kwa maelezo zaidi ni tofauti gani zilizopo kati ya bima inayofuata sheria za kiIslam na ile isiyofuata sheria za kiIslam wasiliana na http://ijuebankyakiislam.blogspot.com



THOMSON REUTERS WAMEZIDI KUIPA NGUVU ISLAMIC INTERBANK BENCHMARK RATE (IIBR)

Thomson Reuters imetangaza uteuzi mpya wa body inayoshughulikia Islamic Interbank Benchmark Rate (IIBR). Tangazo hilo lilitolewa kwenyemkutano wa nane unaojulikana kama Annual World Islamic Fund and Financial Markets Conference ambao unafanyika mwezi wa tano kila mwaka nchini Bahrain. Ktk uchaguzi huo idadi ya wawakilishi waliongezwa ktk IIBR sharia Committee na Islamic Benchmark Committee.

IIBR ilianzishwa mwaka 2011 kama kigezo cha kwanza kinachofuata sheria za kiIslam ambacho kilikua ni kama mbadala ya kigezo kisichofuata sheria za kiIslam kama vile London Interbank Offered Rate (LIBOR). Msomi mashuhuri ambae ameshamaliza muda wake Muhammad Taqi Usman ambae pia ni mwenyekiti wa Accounting and Auditing Organization for Islamic Financial Institutions (AAOIFI) na Sheikh Dr Akram Laldin mkurugenzi mkuu wa International Shariah Research Academy waliingizwa kwenye IIBR Sharia Committee. Justice Taqi Usman atachukua nafasi ya mwenyekiti aliemaliza muda wake Sheikh Talal DeLorenzo ambae atabakia kua Committee member.

Pamoja na mambo mengine Dr Abbas Mirakhor ambe ni mwenyekiti wa uchumi wa unaofuata sheria za kiIslam wa International Centre of Education in Islamic Finance (INCEIF) na Ismail E Dadadhoy ambae ni banker anaejitegemea, mkurugenzi mkuu na mkuu wa uchumi wa Kiislam kwenye benki kubwa kuliko zote nchini Switzerland UBS amechaguliwa kwenye Benchmark Committee.

Sheikh Dr Akram Laldin alinukuliwa akisema ‘nina imani kubwa kwamba IIBR ni hatua nzuri yenye malengo ya kuukomboa uchumi wa kiIslam kutegemea na kigezo kisichofuata sheria za kiIslam ambacho kitu ambacho kimelalamikiwa sana na uchumi unaofuata sheria za kiIslam’. Kwa maelezo zaidi kuhusu uchumi unaofuata sheria za kiIslam soma http://ijuebankyakiislam.blogspot.com


THE TIMES OF INDIA, Jul 31, 2012

Nafasi nyingi za kazi kwenye Benki zinazofuata sheria za kiislam nchini India


Soko kubwa limejitokeza nchini India na nchi nyingine nyingi kwenye secta ya benki zinazofuata sheria za kiIslam na karibu wataalam 50.000 wanahitajika. Kuna haja kubwa ya kupatikana kinachojulikana kama nguvu kazi (human capital) hususan ktk mji wa Hyderabad nchin India.

Akizungumza ktk mkutano wa kuzungumzia maswala ya banki za kiIslam M S Sherrif wa Institute of Islamic Banking Finance and Insurance (IIBFI) alisema. Kuna nchi 75 duniani ambazo zinazitambua benki zinazofuata sheria ya kiIslam ikiwemo south Africa, USA, Singapore, Saudi Arabia, Malaysia na nyinginezo. Benki kubwa duniani zikiwemo HSBC, Citigroup, Deutsche Bank na Standard Chartered zimefungua Islamic windows. Kuna nafasi nyingi za kazi kwa vijana ktk secta hii.

Pamoja na mambo mengine Mr Sherrif alinukuliwa akisema kwamba wasomi ktk secta hiyo wanatakiwa waufahamu vizuri mfumo wa kiuchumi ule unaofuata sheria za kiIslam na ule usiofuata sheria za kiIslam ili wawe ktk nafasi nzuri ya kujibu maswali hususan yale yanayohusiana na riba (interest) ktk mikopo na akiba. Upande mwingine ni ule unaohusu wataalam wa benki zinazofuata sheria za kiIslam wanaohitajika ktk uongozi wa juu.

Reference

Available from http://articles.timesofindia.indiatimes.com/2012-07-31/hyderabad/32960574_1_deutsche-bank-islamic-shariq-nisar [Accessed 29/07/2012].





Bank Muamalat ya Malysia imesaini memorandum of understanding (MoU) na China banking group

Bank Muamalat Bhd ya Malaysia na Bank of Shi Zui Shan ya China zimesaini memorandum of understanding (MoU) ya ushirikiano kwa ajili ya kuanzisha bank zinazofanya kazi kwa kufuata mfumo wa sheria za kiIslam nchini China.

Mkurugenzi mkuu wa Bank Muamalat Datuk Mohd Redza Shah Abdul Wahid akifafanua uhusiano huo alisema, bank mbili hizo zina matumaini ya kuanzisha benki zinazofuata sheria ya kiIslam ktk kipindi cha miaka miwili inayokuja. Ktk hatua za mwanzo, makundi hayo mawili yatabadilishana utaalam na kutakua na mafunzo maalum yanayohusu bank za kiIslam.

Vitengo karibu 23 vya benki zinazofuata sheria ya kiIslam vitaanzishwa ktk mikoa mbalimbali nchini Humo ktk kipindi cha mwaka mmoja. Kufuatia kuanzishwa kwa vitengo hivyo, itapatikana nafasi ya kuzijaribu banki hizo na baadae kufungua benki ambayo itakua ni benki kamili ya kiIslam. Ushirikiano huo ni moja kati ya juhudi za makusudi za serikali ya China kuhamasisha bank zinazofuata sheria ya kiislam.

Bank Muaamalat itawafanyia mafunzo ya banki zinazofuata sheria za kiIslam wataalam watano wa Benki ya Shi Zui Shan na gharama zote za mafunzo hayo zitatolewa na Benki Muamalat. Pamoja na mambo mengine wataalam wa Benki Muamalat watatoa huduma ya ushauri kwa Benki ya Shi Zui Shan ktk kipindi chote cha kukua kwa benki hiyo.

China ina idadi ya waIslamu wasiopongua milioni 30 na wengi wao wanaishi Ningxia mji ambao upo Yinchuan na kuna soko kubwa ambalo pande zote mbili zinamategemeo ya kufaidika nalo.

Reference

http://biz.thestar.com.my/news/story.asp?file=/2012/7/21/business/11703480&sec=business



Waziri wa Ireland anaukaribisha uchumi unaofuata sheria za kiIslam

Uchumi unaofuata sheria za kiIslam unakaribishwa nchini Ireland amesema waziri wa mambo ya jamii wa Ireland Miss Joan Burton. Waziri ameyasema hayo kwenye mkutano wa kimataifa unaohusu masuala ya uchumi na ujasirimali unaofuata sheria za kiIslam ulioandaliwa na Irish Business Executice Forum (IBEF). Waziri huyo alinukulia akisema ‘Serikali imeweka misingi itakayoziwezesha uchumi unaofuata sheria za kiIslam zikiwemo benki za kiIslam kutambulika.

Aliongeza kwamba tunafahamu kwamba kazi kubwa bado inatakiwa ifanyike hususan ktk nchi ambayo kuna changamoto nyingi za kiuchumi. Tuna sheria nyingi zinazohusiana na swala zima la uchumi wa kiIslam na kuna yale maswala yanayohusiana na sheria za kiuchumi za benki kuu ya Ireland. Waziri amesisitiza kwamba kuna sheria ambazo zitabidi ziongezwe ktk wakati wa baadae ili taasisi za kiislam ziweze kufanya kazi zake kwa ufanisi. Waziri mwengine wa Ireland Mr Tom Woods amefafanua kwamba uchumi wa kiIslam ni moja kati ya area inayokua sana ktk soko la kiuchumi duniani na serikali yake imeahidi kufanya kila linalowezekana kwa ajili ya kuindeleza sector hiyo nchini Ireland. Akilielezea hilo kwa ufasaha zaidi alikumbusha kwamba mwaka 2008 kulianzishwa timu maalum nchini Ireland ambayo imebobea ktk maswala ya uchumi wa kiIslam kwa ajili ya kulishughulikia swala hilo.

Dr. sheikh shaheed Sataedien President of Muslim council of Ireland na (IBEF) aliuliza baadhi ya maswali kam vile je inawezekana uchumi kukua na wakati huohuo tukaendela kuhifadhi mazingira, vipi serikali zinaweza kuongeza kipato inachokihitaji kwa ajili ya huduma za afya, jamii, na nyenginezo, nini hasa serikali inatakiwa ifanye ktk uchumi wan chi, je tutakuwa ktk hali nzuri zaidi kimaisha kama kodi zikipunguzwa na maswali mengine mengi. Kwa maelezo zaidi kuhusu benki zinazofuata sheria za kiIslam ingia www.ijuebankyakiislam@blogspot.com



Riba (interest) ya LIBOR yaiweka pabaya Barclays bank

London Interbank Offered Rate (LIBOR) ni makadirio ya kiwango cha riba kinachotumika wakati benki zinapokopeshana pesa. Kiwango hicho cha riba kinatumiwa na mabenki yanapokopeshana kwa kulipa mikopo ya muda mfupi na muda mrefu (siku moja, mwezi hadi mwaka) Kiwango hicho kinawekwa na British Bankers’ Association (BBA) kila siku saa tano asubuhi kwa time za Uingereza.

Taasisi za pesa wanapotoa mikopo, credit card au (Mortgage) kumkopesha mteja nyumba, wanawatoza wateja kiwango cha riba kulingana na kile kiwango cha riba kilicho pangwa na BBA (LIBOR) au wanaongeza zaidi. LIBOR kwa kawaida inatumika kama kigezo (benchmark) cha kiwango cha riba kwa pound ya kiingereza na sarafu za nchi nyingine nyingi. Kinachofanyika ni kwamba kila siku, benki 16 zinatakiwa zitaje kwa wawakilishi wa mabenk (BBA) kiwango cha riba (borrowing cost) kinachotozana pindi mabenki hayo yanapo kopeshana.

LIBOR imezusha mjadala mkubwa kuhusu uhalali wake na vigezo inavyovitumia ktk kufanya kazi kwake, kwa mfano gavana wa bank ya England Mervyn King ameripotiwa akisema ‘wakati umefika kwa LIBOR kubadilsha utendaji wake wa kazi kutoka kwenye makadirio na kwenda kwenye kuangalia jinsi soko la biashara lilivyo ili kujua vipi riba inaweza kukadiriwa.

Moja ktk vitu ambavyo vimekua na mshituko mkubwa kuhusiana na utumiaji wa Libor ni pamoja na ile ya kutozwa faini ya pound 290 million Barclays bank kwa kile kilichodaiwa kwamba kwa makusudi wameweka kiwango maalum cha LIBOR (kufix) kwa maslahi ya bank hiyo. Kwa mujibu wa taarifa rasmi mbalimbali ambazo zilizoandaliwa Marekani na uingereza zimeeleza kwamba, kulikua na mazungumzo kati ya viongozi wa juu wa Barclays na viongozi wa mabank mengine ambapo ilidawa kua bank nyingine zilionyesha wasiwasi wao kutokana na kiwango cha riba cha Barclays kua juu ukilinganishe na kile cha bank nyingine.

Kufuatia maelezo hayo tumeona ipo haja ya kulizungumzia swala zima la LIBOR kwa ujumla na uhusiano wa LIBOR na bank za kiislam kwa ufupi. Tukirudi kwa upande wa bank za kiIslam, wasomi wengi wameonyesha waiwasi wa kutumia LIBOR kwa sababu kuna mazingira ya riba ambayo hayakubaliki kisheria. Pamoja na mambo mengine, mwaka 2011 Islamic bank ilifanikiwa kupata the Islamic Interbank Benchmark Rate (IIBR). Kwa ufupi, IIBR ni kiwango cha faida ambacho kinakubalika na Mabank kwamba kimekamilisha masharti yanayokubalika na sheria ya kiIslam, Mabank yanafanya hivyo kwa kukubali kutoa na kupokea kiwango hicho kulingana na hali halisi ya soko la biashara. Makadirio ya kiwango hicho yanafanyika kabla kidogo ya saa tano asubuhi kwa taimu za Makkah ambayo ni sawa na taimu za (GMT + 3).

Kinachotokea ni kwamba kinanyakuliwa kiwango cha Mabank 16 na Thomson Reuter saa 10. 45 AM kila siku kuanzia Jumapili mpaka Al khamis. Bank zinaombwa zitaje kiwango chao kati ya saa 9.00 AM- 10.44 AM kwa taimu za Makkah ,na zinatakiwa zijibu maswali yafuatayo. Ni kiasi gani cha faida yatapenda kushiriki kwa ajili ya inter-bank ambayo inafuata sheria ya kiislam na je yatakubali kuuza na kununua kwa kiwango hicho kwa muda wa siku moja au wiki moja na kuendelea. Baada ya hatua hiyo, Thomson Reuters inajiridhisha kwamba utaratibu umefuatwa kwa kufanya audit na kwa kuhakikisha kwamba kiwango kilichotajwa ni sahihi na wanachukua wastan utakaopatikana ktk Mabank hayo 16 na kiwango hicho kinatumiwa kupatikana IIBR. Tofauti nyingine ni ile ya sheria ya kiislam kuzuia kamari (speculation) na hadaa (gharar), na kuzuia biashara ambazo sio halali kisheria. Faida ya mtaji ktk uchumi wa kiIslam inategemea jinsi gani mjasirimali atakua tayari kukubali hasara inayotokana na biashara na sio kutegemea riba. Upande mwingine ni ule unaohusiana na kuuza deni pamoja na kutaka uhakika (guarantee) ya faida, hilo haliruhusiwi ktk sheria ya kiIslam na badala yake mifumo mingine ya kibiashara inaweza kutumika kama vile Mudarabah na musharakah.

Kufuatia scandal ya LIBOR bado inaendelea na kuna uwezekano mkubwa wa kuchukua muelekeo mwengine kabisa ktk wakati wa baadae lakin hadi sasa, mwenyekiti wa Barclays Marcus amejiunzulu Jumatatu ya tarehehe 2/07/2012 na mkurugenzi (Chief executive) wa Barclays Bob diamond nae amejiunzulu kufuatia shinikizo la wanasiasa. Kwa maelezo zaidi na ushahidi wa hayo soma www.ijuebankyakiislam@blogspot.com


Bibliography


Burne, K. (2011), Islamic Banks Get a ‘Libor’ of Their Own. Available from http://online.wsj.com/article/SB10001424052970204443404577054150155788364.html [Accessed 30/06/2012].

Divanna, J. (2010), Islamic rate of return: the new IRR. Available from http://www.islamic-banking.com/resources/7/NewHorizon%20Previouse%20Issues/NewHorizon_July-Sept-10.pdf [Accessed 28/06/2012].

http://www.dailymail.co.uk/news/article-2167458/Libor-Dispute-said-Mervyn-Kings-deputy-senior-Barclays-boss.html#ixzz1zRw3JT4z [Accessed 01/07/2012].
http://www.bbc.co.uk/news/business-18685040 [Accessed 02/



 Tatizo la LIBOR
 
London Interbank Offered Rate (LIBOR) ni makadirio ya kiwango cha riba kinachotumika wakati bank zinapoazimana pesa. Kiwango hicho cha riba kinahisabiwa kwa vipindi tofauti kuanzia siku moja, wiki moja, mwezi mmoja, miezi miwili hadi miezi sita. Kiwango hicho kinatangazwa na British Bankers’ Association (BBA) kila siku saa tano asubuhi kwa time za Uingereza. Taasisi nyingi za uchumi, wakopeshaji, watoaji wa credit card wanatoa kiwango chao cha riba kulingana na kile cha LIBOR au zaidi.

LIBOR kwa kawaida inatumika kama kigezo (benchmark) cha kiwango cha riba kwa pound ya kiingereza na pesa za nchi nyingine nyingi zikiwemo dola, Euro, Yen ya kiJapan, frank ya Uswizi, Dola ya Canada, New Zealand na Australia, Krona ya Uswizi na Danish. Kiwango cha LIBOR kinahisabiwa kwa kutumia sarafu mbalimbali kila bank inatoa makadirio yake kwa kutegemea gharama ya jinsi walivyoazima (borrowing costs).

Tatizo lililopo hasa ni lile linalodaiwa kwamba Barclays bank imezusha (manipulate) kiwango cha riba ambacho bank zinakopeshana. Tatizo hilo limepelekea watu kadhaa kujiunzulu nyazifa zao akiwemo mtendaji mkuu (chief excutive) Bob Diamond na mwenyekiti wa Barclays ndugu Marcus Aguis. Ni mapema kujua maelezo kamili na athari itakayotokea kwani mambo mengi bado hayajakua wazi. Tutalifafanua tukio hilo zaidi hapo baadae.


 Pakistan na Iran

Huko Pakistan inaripotiwa kua serikali ya nchi hiyo imefungua milango kwa mashirika ya ujenzi wa bomba za gasi kupeleka maombi ya kupata zabuni za ujenzi wa bomba la gasi linalotarajiwa kusafirisha gasi kati ya nchi mbili hizo. Wataalam wa kiuchumi wa nchi mbili hizo wanadai kwamba ujenzi wa bomba hilo ukikamilika utaiwezesha Iran kuipatia Pakistan kiasi cha mitre 8.7 trillion za gasi kwa kipindi cha miaka 25. Matangazo haya yanakuja katika kipindi ambacho Marekani na Ulaya Magharibi imeweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran. Kwa upande mwengine wataalamu wa kiuchumi nchini Pakistan wanaona ya kwamba mpango huu utaifaidisha sana nchi hiyo yenye urafiki wa karibu na Marekani.


Iraq

Katibu mkuu wa baraza la mawaziri la nchi hiyo Ally al-Yilaq ameilaumu sana bank kuu ya nchi hiyo kwa kuhusika na usafirishaji haramu wa karibu 180 trilions za Iraq ambazo ni sawa na $138.5 million katika kipindi kifupi kilichopita,imedaiwa kua chanzo chake ni kutokana na bank hiyo kutokua makini na kazi zake za kila siku. Wakati huo huo imeripotiwa kua thamani ya pesa ya nchi hiyo inaendelea kushuka kwa kasi, habari ambayo imethibitishwa na mkaguzi mku wa fedha wa serekali ya Iraq.

Marekani

Habari kutoka Marekani(USA) zinaeleza kua ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo umezidi kudorora katika robo ya kwanza ya mwaka 2012 kitu ambacho kinatishia pia ukuaji wake hapo siku za baadae. Imeripotiwa kua suala la uchumi linategemewa kuchukua nafasi kubwa katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo hapo mwezi November mwaka huu. Inasemekana kua nusu ya wapiga kura wa nchi hiyo wanadai kua suala la uchumi ndio litaamua nani atakua mshindi katika uchaguzi unaokuja.


Wizara ya Mafuta ya Iraq imeutuhumu uongozi wa Kurdistan kwa kusafirisha kwa njia zisizo rasmi kiasi kikubwa cha mafuta yasiyosafishwa na kuyapeleka nchi jiran kama vile Iran na Afganistan. Wakati huo huo Kurdistan imetangaza kusitisha uzalishaji mafuta kutokana na matatizo ya kiumiliki wa mafuta kati ya serikali kuu ya Iraqi na ile ya Kurdistan.

Imeripotiwa kua Waziri wa Nishati na Madini wa Kurdistani ndugu Ashter Horami, amedai kua Kurdistan haitasafirisha wala kuzalisha mafuta kwa Iraq mpaka hapo watakapotatua matatizo yaliyopo kati yao. Alidai kua kuna matatizo mengi ya kibiashara hasa yale yanayohusiana na madeni ya nyuma ambayo Kurdistan inaitaka Iraq iyalipe kabla ya kusafirisha mafuta mengine zaidi kwa Iraq. Waziri huyo alidai kua serikali ya Iraq inataka ichukue mafuta kutoka Kurdistan bila kulipa chochote jambo ambalo linapingwa vikali na serikali ya Kurdistan.

Huko Sudan

Habari nyingine za kiuchumi ambazo zimechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari ni zile za kushambuliwa kwa mabomba ya kusafirishia mafuta huko sudan ya kusini. Habari za kuaminika ni kwamba mabomba hayo yalishambuliwa na ndege za kivita za sudan ya kaskazini. waandishi wa habari waliomiminika katika eneo hilo tangia kuanzia kwa mvutano kati ya Sudan hizo mbili, wamedai kua tukio hilo ni la kichokozi lisiloweza kuvumiliwa kabisa. Idadi ya waliopoteza maisha katika shambulio hilo haikuweza kujilikana mara moja, isipokua maiti kadhaa za majeshi ya pande zote mbili zilizagaa katika eneo la tukio. Imeripotiwa kwamba watu kadhaa waliokimbia makazi na kelekea kwenye kambi za wakimbizi zilizo karibu na eneo la tukio. Hata hivyo msemaji wa majeshi ya Sudan kaskazini Kanal Khaleed Saad Al-wasani amekanusha vikali kutokea kwa tukio hilo, na amedai kua sio majeshi ya sudan yaliyopitisha shambulio hilo.


Gari ya kutumia umeme

Taarifa kutoka BBC London zinaeleza kwamba shirika la magari la Vauxhall limetengeneza gari inayotumia umeme badala ya petrol au diesel na gari hiyo inajulikana kama Vauxhall Ampera.

Hii inakuja baada ya muuzaji mkuwa wa gari za umeme nchini uingereza Nissan Leaf ambae gari zake ni sawa na pound 26,000 za kiingereza sawa na takriban 65,000,000 Shilingi za Tanzania. Wakati huohuo gari nyingine ya kutumia umeme inayojulikana kama Renault Fluence itaingia madukani nchini uingereza kwa bei ya pound 17,000 sawa na shilingi takriban 4,250,000 za Tanzania. Moja kati ya sifa ya gari hizo ni kua dereva ananunua gari na anakodisha betrii tofauti, ambapo betrii itamgharimu kiasi cha pound 1000 kwa mwaka, sawa na pesa za Tanzania shilingi 250,000, ispokua kwa bei hiyo utakua huna haja ya kununua betrii nyingine tena.

Ni muhimu kufahamishana kwamba gari hiyo itakua na uwezo wa kutembea maili 150 sawa na kilometa 200 lakin kwa uhakika zaidi unaweza kuendesha kati a maili 70 mpaka 80 na inahitaji kuichaji betrii kwa muda wa masaa manane. Sio gari ambayo kila mtu anaweza kuitumia alisema Andy Heiron ambae ni mkuu wa kitengo cha gari za umeme nchini uingereza.

Bado tatizo la kilometa kidogo ambazo gari hiyo ina uwezo wa kuendeshwa linaonekana kuitishia biashara hiyo, lakin kama mtu anataka kuendesha zaidi ya kilometa zilizotajwa, anaweza kununua Nissan Ampera ambayo pamoja na kwamba itakua na uwezo wa kwenda mile 20 mpaka 50 kwa kutumia betrii peke yake, bado itakua imeambatanishwa na genereta ambayo itajiwasha yenyewe baada ya betrii kumaliza chaji yake, na baada ya hapo itakua na uwezo wa kutembea kwa kutumia genereta hadi maili 350. Kuna mpango wa muda wa kuchaji betrii ya gari hiyo kupunguzwa hadi kufikia muda wa saa moja kutoka masaa manane kama ilivyo sasa.


Huko Ulaya Magharibi

Benk kuu ya Ulaya imeonya kua kuna hatari ya kutokuwepo na utulivu wa kiuchumi katika eneo la ulaya. Jumla ya dalili hizo ni pamoja na kupanda mno kwa bei za bidhaa na kubakia mishahara kama ilivyo kitu kinachofahamika kama (inflation). Kwa upande mwengine huko Ureno habari zilizoenea ni kwamba kuna taarifa rasmi za kuionya nchi hiyo kua, ipo haja ya kuwa na mpango mpya maalumu wa kuokoa uchumi wa nchi hiyo baada ya ile mipango ya kwanza iliyofanywa mwaka 2011 kuonekana kua haikumaliza tatizo hilo. Piter Vies ambae ni mjumbe maalum katika mambo ya kiuchumi wa nchi za Ulaya na ambae pia ni mjumbe katika shirika la misaada la kifedha Duniani , aliweka wazi kua suala hili la kufanya marekebisho katika uchumi wa Ureno, linakuja katika wakati ambao nchi hiyo haijapiga hatua yoyote kiuchumi.

Umeme wa nguvu za jua

Nguvu za jua katika kuzalisha umeme kwa matumizi ya binadamu inaonekana ni suala ambalo hakuna budi kulieleza kwa ufasaha zaidi na umuhimu wake hauna mjadala. Hayo yamesemwa na wataalamu wa nguvu za umeme katika mkutano wao uliofanyika huko Doha mji mkuu wa Qatar. Wataalamu hao wameonya ya kwamba kutegemea moja kwa moja umeme unaozalishwa na mafuta ya Petrol, kunatishia mafuta yenyewe kutoweka ifikikapo mwaka 2015, hii inatokana na kukua kwa matumizi na mahitaji ya mafuta.

Kufuata mfumo wa sheria ya kiislam kunanyanyua kiwango cha biashara kwa asilimia 25%

Gazeti linaloshughulikia mambo ya biashara nchini United Arab Emirates (UAE) linalojulikana kama Zawya limeripoti kwamba kuigeuza biashara kutoka ktk mfumo wa kawaida na kuipeleka kwenye mfumo wa kufuata sheria na maadili ya kiislam kunaweza kuongeza thamani ya shirika kwa asilimia 18-25 Imesema Swiss Banking Group, Bank Sarasin. Iliyasema hayo wakati ilipokua inatoa ripoti yake inayojulikana kama Islamic Wealth Management report. Ilieleza repoti hiyo kwamba wakati utaratibu wa mageuzi hayo unahitaji juhudi kubwa kuanzia kwenye miondo mbinu, mpaka kufikia uzalishaji na zaidi, ikiwemo vipi shirika litatumia faida yake, bado soko la biashara hiyo ni kubwa hasa ukizingatia kuwa idadi ya waislam inategemewa kuongezeka kwa asilimia 26 mpaka mwaka 2030 ambapo idadi ya waislam inategemewa kufikia watu billion 2.2 duniani. Soko la huduma za kiislam linategemewa kushindana na soko la China na India kwa ukubwa.

Bank Sarasin ni bank binafsi ambayo ina uzowefu wa miaka mingi na inatoa huduma zenye kiwango cha hali ya juu na ina wataalam wenye kiwango cha juu. Kazi yake ni pamoja na kutoa ushauri ktk maswala ya uwekezaji, kusimamia rasilimali kwa kampuni binafsi na mashirika mbambali.


Serikali ya Uturuki imeonyesha nia yake ya kutaka kuuza dhamana (Bonds) za kiislam kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa gazeti linalotoka nchini Uingereza linalo julikana kama ‘Global Islamic Finance Magazine’, Serikali ya Uturuki imetangaza utaratibu wa kutoa dhamana za kiislam kwa mara ya kwanza baada ya ubishi uliodumu kwa muda mrefu. Moja ya sababu ya kuchukua uamuzi huo ni pamoja na kuongezeka mapato ya nchi hiyo kwa sababu ya kuongezeka mapato yanayotokana na sekta ya mafuta. Naibu waziri mkuu wa Uturuki Ali Babacan ametangaza nia ya serikali yake kuhusu swala hilo. Hatua hiyo inaonyesha nia ya Uturuki kutaka kua kiungo muhimu cha banki za kiislam pamoja na kua serikali yake sio ya kiislam tokea mwaka 1923. Soko la ulimwengu la dhamana za kiislam linakadiriwa kufikia dola million mia moja za kimarekani.


Bank ya kiislam ya ABC imetangaza faida ya dola za kiMarekani million 8.1.

Manama, Bahrain: Banki ya kiislam ya ABC imetangaza faida ya dola za kiMarekani million 8.1 kwa mwaka wa 2011 ambapo ni kiwango cha juu kwa asilimia 293% kuliko mwaka uliopita. Jumla ya gharama za uendeshaji zilikua ni dola za kiMarekani 15.1 million ukilinganisha na dola za kiMarekani 15.9 mwaka 2010.

Bank za kiislam zimeamua kufuata ubia (partnership) kama ufumbuzi.

Imeripotiwa kwamba bank za kiislam dunia nzima zinataka kufuata utaratibu wa ubia (partheship) kama aina ya uchumi wake haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kumaliza tatizo la gharama linalojulikana kama foreign bill purchase (FBP) na gharama nyingine zinazojulikana kama inland bill purchase (IBP). Ni uhakika usiopingika kwamba bank za kiislam zinakua kwa kasi ktk soko la kimataifa, kwa mfano kuna bank za biashara saba nchini Bangladesh ambazo zinafanya kazi zake kwa kufuata kikamilifu sheria ya kiislam wakati bank nyingi za kigeni nchini humo zina huduma za bank za kiislam.

No comments:

Post a Comment