Tuesday, 3 April 2012

Matatizo ya uchumi na ufumbuzi wake kwa kutumia uchumi wa kiislam

Vipi uchumi wa kiislam unaweza kusaidia matatizo ya kiuchumi yanaoendelea duniani

Matatizo ya kiuchumi ni matokeo ya mipangilio mibaya ya kiuchumi ambayo inashindwa kumbebesha majukumu kila mmoja ktk jamii. Mafanikio ya uchumi wowote yanategemea uwiano kati ya maadili na mahitaji ya binadamu, mshikamano wa vitu viwili hivyo ndio ambao unajenga misingi ya uchumi wa kiislam. Kwa upande mwingine kama uhusiano huo hautochungwa vizuri, basi utulivu na uwiyano ktk jamii utakua hauna uhakika. Msingi wa uchumi wa kiislam ni kwamba Mungu ameumba binadamu kama muwakilishi ktk dunia lakin yeye anabaki kua mmiliki halisi wa dunia na vyote vilivomo ndani yake. Pamoja na mambo mengine Mungu amempa binadamu jukumu la kutumia vizuri vilivomo ktk dunia kwa maslahi yake na maslahi ya kizazi kijacho.

Uislam unaliangalia swala la uchumi ktk sura pana zaidi, kwa mfano, Kila kitu ktk biashara kinaruhusiwa kama hakitapingana na vyanzo vyovyote vya sheria ya kiislam ikiwemo Quran, hadith na vinginevyo. Sasa kama utaangalia vizuri matatizo ya kiuchumi ambayo yameukumba ulimwengu na yanaendelea kusumbua, yametokana na sababu nyingi ikiwemo kitu kinachojulikana kama (assert liability mismatch) kitu ambacho kinaishiria hali ya kutokua na uwiano kati ya madeni yanayodaiwa na rasilimali zilizopo, jingine ni pamoja na kufanya maamuzi bila uhakika, kutokua na sheria madhubuti ktk mambo yanayohusiana na fedha na kutumia njia za udanganifu ktk kibiashara. Kwa upande mwengine maadili ya uchumi wa kiislam yanamuamrisha mtu kufanya biashara na mikataba na uhusiano wowote wa kibiashara kwa uadilifu wa hali ya juu sambamba na sheria.

Kuna wale wanaoona kwamba maadili ya uchumi wa kiislam yanamfanya muhusika ashirikiane na anaefanya nae biashara ktk hasara na faida kitu ambacho kinasaidia sana kuhamasisha matajiri kufanya biashara kwa maslahi ya jamii nzima, wakati huohuo zinawabana wale ambao wanakataa uadilifu. Uchumi wa kiislam una malengo ya kuinufaisha jamii nzima na kua na uchumi mzuri kwa kusisitiza uaminifu, uadilifu, uwazi, haki sawa kwa kila mmoja. Uislam hauhimizi kitu ambacho ni kipya sana duniani na kitu ambacho kinawahusu waislam pekeyao. Ninadhani utakubaliana na mimi kwamba binadamu amepambana na anaendelea kupambana na dhuluma na maadili mabaya kwa sababu ni sifa ambayo haina mipaka na kama binadamu akishindwa kupambana na dhuluma, atakua sio tu ameshindwa kujifanyia uadilifu yeye mwenyewe ispokua na wengine

Shamsi (2004) ameripoti akisema kama sheria za kiuchumi za kisasa zikitumika, kutakua na mabadiliko ktk mpangilio wa kiuchumi, kwa mfano ni lazima maswala ya masikin yapewe kipaumbele au baadhi ya biashara zifungwa kwakua zinakwenda kinyume na maadili.

Kwa mantiki hiyo matatizo ya kiuchumi yaliotokea yangeweza kuepukwa kwa kuishawishi jamii kwamba malengo ya uchumi ni lazima yawe na muelekeo unaoendana na maadili kama vile moyo wa ushirikiano ktk jamii na kuepuka ushindani usiokua halali.Mfanya biashara anatakiwa awe muaminifu ambapo atatakiwa ataje aibu zote zilizo ktk bidhaa zake, ukweli ni sifa muhimu sana ktk maadili ya biashara. Kuna sababu nyingi za matatizo ya uchumi wa dunia lakin tumejaribu kwa mukhtasar kuangalia baadhi.

Kwa maelezo zaid unaweza kupitia

Shams, R. (2004). A critical Assessment of Economics. HWWA Discussion, Hamburg: Institute of International Economics. World economic forum. (2010), Faith and the Global Agenda: Values for the Post-Crisis Economy, Geneva.



No comments:

Post a Comment