Baada ya kuelezea historia ya Bank kwa ufupi imeonekana kwamba kuna umuhimu wa kuelezea historia ya pesa kwa sababu ya uhusiano uliopo kati ya pesa na bank. Moja kati ya maswali ambayo yanayoweza yakajitokeza ktk maswala mazima ya historia ya pesa ni pamoja na swali kwamba kipi kilianza kutumika mwanzo kati ya pesa na bank wakati moja kati ya maoni ni kua bank zilianza kutumika mwanzo kuliko pesa.
Itakumbukwa kua Pesa ilianzia kwenye mfumo wa mawe, dhahabu, shaba mpaka kuifikia noti. Hii yote ilitokana na mahitaji ya binadamu kupata kitu ambacho ni mbadala wa kubadilishana bidhaa kwa bidhaa. Mfumo huu wa kubadilishana bidhaa kwa bidhaa nyingine ulisababisha usumbufu mkubwa kama ule uliotokana na usafiri, uharibifu wa bidhaa na mengineyo. Tulieleza ktk makala zilizopita kwamba kawaida ya tamaduni ni kuhama kutoka eneo kwenda eneo nyengine. Utamaduni wa pesa nao ulianzia katika dola la Persia kisha ukatambaa kwengineko kama vile China, Egypt, Ugiriki na Uholanzi.
Historia inaonyesha kua Pesa ktk picha hii tuliyonayo sasa, ilianzia Egypt na Mesopotamia miaka mingi kabla ya kuzaliwa nabii Issa ambayo inajulikana kama (BC) Wakati huo watu walitumia dhahabu kama pesa. Pia inadaiwa kua Sarafu ya kwanza ilitengenezwa Uturuki miaka 650 BC nayo ilitengenezwa kwa kutumia dhahabu na shaba.Wanahistoria wengi wa masuala ya fedha wanakubaliana kua Noti ya kwanza ilitenngenezwa China ktk nchi za Asia. Kwa upande wa Ulaya Noti ya kwanza ilichapishwa Sweden na baadae Ufaransa.
Ambalo linafahamika ni kwamba fedha ya nchi yoyote inatiwa thamani kwa dhahabu lakini wakati not zilipoanza kutumika hazikua zikilindwa kwa kutiwa thamani na kitu chochote. Kwa sababu hiyo noti zilishindwa kuendelea na zilipoteza thamani yake. Ktk karne ya 18 bank ya kila nchi ilianza kuchapisha noti ambazo zililindwa kwa ahadi ya serikali kua zina thamani ya dhahabu kitu ambacho kiliifanya pesa ya noti kuaminika.
Marekani ilisimamisha kutia kiwango cha pesa zake kwa kutumia dhahabu mwaka 1933 na ikahamia kwenye mfumo unaojulikana kama (Exchange rate) mwaka 1971. Jumanne iliyopita mkuu wa federal reserve ya Marekani Bernanke aliutetea uamuzi huo kwa kusema kua kutumia dhahabu kwa ajili ya kutilia thamani pesa ni matumizi mabaya ya vyanzo vya uchumi.
Alinikuliwa akisema kama unataka kua na gold standard inakubidi uende Africa ya kusini au baadhi ya nchi nyingine kwenda kuchimba dhahabu na baadae uilete New York kwa ajili ya kuihifadhi kitu ambacho kinahitaji juhudi kubwa.
No comments:
Post a Comment